Isaya 5:27
Isaiah 5:27 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Hakuna hata mmoja wao anayechoka wala kujikwaa, hakuna hata mmoja anayesinzia wala kulala, hakuna mkanda uliolegezwa kiunoni, hakuna gidamu ya kiatu iliyokatika.
Isaiah 5:27 in English
Isaiah 5:27 · Berean Standard Bible
None of them grows weary or stumbles; no one slumbers or sleeps. No belt is loose and no sandal strap is broken.
Context
25Kwa hiyo hasira ya Bwana inawaka dhidi ya watu wake,
mkono wake umeinuliwa na anawapiga.
Milima inatetemeka,
maiti ni kama takataka kwenye barabara.
Hata kwa haya yote, hasira yake haijageukia mbali,
mkono wake bado umeinuliwa juu. 26Yeye anainua bendera kwa ajili ya mataifa yaliyo mbali,
anapiga filimbi kwa ajili ya wale walio kwenye miisho ya dunia.
Tazama wamekuja,
kwa kasi na kwa haraka! 27Hakuna hata mmoja wao anayechoka wala kujikwaa,
hakuna hata mmoja anayesinzia wala kulala,
hakuna mkanda uliolegezwa kiunoni,
hakuna gidamu ya kiatu iliyokatika. 28Mishale yao ni mikali,
pinde zao zote zimevutwa,
kwato za farasi wao ziko kama jiwe la gumegume,
magurudumu ya magari yao ya vita ni kama upepo wa kisulisuli. 29Ngurumo yao ni kama ile ya simba,
wananguruma kama wana simba,
wanakoroma wanapokamata mawindo yao,
na kuondoka nayo pasipo yeyote wa kuokoa.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.