Native Bible

Isaiah 5:22 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Ole wao walio mashujaa kwa kunywa mvinyo, nao walio hodari katika kuchanganya vileo,

Isaiah 5:22 in English

Isaiah 5:22 · Berean Standard Bible

Woe to those who are heroes in drinking wine and champions in mixing beer,

Context

20Ole wao wanaoita ubaya ni wema, na wema ni ubaya, wawekao giza badala ya nuru, na nuru badala ya giza, wawekao uchungu badala ya utamu, na utamu badala ya uchungu. 21Ole wao walio na hekima machoni pao wenyewe, na kujiona wenye akili machoni pao wenyewe. 22Ole wao walio mashujaa kwa kunywa mvinyo, nao walio hodari katika kuchanganya vileo, 23wale wanaoachilia wenye hatia kwa kupokea hongo, lakini huwanyima haki wasio na hatia. 24Kwa hiyo, kama ndimi za moto zirambavyo nyasi, na kama vile majani makavu yazamavyo katika miali ya moto, ndivyo mizizi yao itakavyooza na maua yao yatakavyopeperushwa kama mavumbi; kwa kuwa wameikataa sheria ya Bwana Mwenye Nguvu Zote na kulisukumia mbali neno la Aliye Mtakatifu wa Israeli.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.