Isaya 5:20
Isaiah 5:20 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ole wao wanaoita ubaya ni wema, na wema ni ubaya, wawekao giza badala ya nuru, na nuru badala ya giza, wawekao uchungu badala ya utamu, na utamu badala ya uchungu.
Isaiah 5:20 in English
Isaiah 5:20 · Berean Standard Bible
Woe to those who call evil good and good evil, who turn darkness to light and light to darkness, who replace bitter with sweet and sweet with bitter.
Context
18Ole wao wanaovuta dhambi kwa kamba za udanganyifu
na uovu kama kwa kamba za mkokoteni, 19kwa wale wanaosema, “Mungu na afanye haraka,
aharakishe kazi yake ili tupate kuiona.
Huo mpango wa Aliye Mtakatifu wa Israeli na ukamilike,
tena udhihirike ili tupate kuujua.” 20Ole wao wanaoita ubaya ni wema,
na wema ni ubaya,
wawekao giza badala ya nuru,
na nuru badala ya giza,
wawekao uchungu badala ya utamu,
na utamu badala ya uchungu. 21Ole wao walio na hekima machoni pao wenyewe,
na kujiona wenye akili machoni pao wenyewe. 22Ole wao walio mashujaa kwa kunywa mvinyo,
nao walio hodari katika kuchanganya vileo,
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.