Isaya 5:18
Isaiah 5:18 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ole wao wanaovuta dhambi kwa kamba za udanganyifu na uovu kama kwa kamba za mkokoteni,
Isaiah 5:18 in English
Isaiah 5:18 · Berean Standard Bible
Woe to those who draw iniquity with cords of deceit and pull sin along with cart ropes,
Context
16Lakini Bwana Mwenye Nguvu Zote atatukuzwa
kwa ajili ya haki yake,
naye Mungu Mtakatifu atajionyesha mwenyewe
kuwa mtakatifu kwa haki yake. 17Kondoo watajilisha kwenye malisho yao wenyewe,
wana-kondoo watajilisha katika magofu ya matajiri. 18Ole wao wanaovuta dhambi kwa kamba za udanganyifu
na uovu kama kwa kamba za mkokoteni, 19kwa wale wanaosema, “Mungu na afanye haraka,
aharakishe kazi yake ili tupate kuiona.
Huo mpango wa Aliye Mtakatifu wa Israeli na ukamilike,
tena udhihirike ili tupate kuujua.” 20Ole wao wanaoita ubaya ni wema,
na wema ni ubaya,
wawekao giza badala ya nuru,
na nuru badala ya giza,
wawekao uchungu badala ya utamu,
na utamu badala ya uchungu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.