Isaya 5:23
Isaiah 5:23 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
wale wanaoachilia wenye hatia kwa kupokea hongo, lakini huwanyima haki wasio na hatia.
Isaiah 5:23 in English
Isaiah 5:23 · Berean Standard Bible
who acquit the guilty for a bribe and deprive the innocent of justice.
Context
21Ole wao walio na hekima machoni pao wenyewe,
na kujiona wenye akili machoni pao wenyewe. 22Ole wao walio mashujaa kwa kunywa mvinyo,
nao walio hodari katika kuchanganya vileo, 23wale wanaoachilia wenye hatia kwa kupokea hongo,
lakini huwanyima haki wasio na hatia. 24Kwa hiyo, kama ndimi za moto zirambavyo nyasi,
na kama vile majani makavu yazamavyo katika miali ya moto,
ndivyo mizizi yao itakavyooza
na maua yao yatakavyopeperushwa kama mavumbi;
kwa kuwa wameikataa sheria ya Bwana Mwenye Nguvu Zote
na kulisukumia mbali neno la Aliye Mtakatifu wa Israeli. 25Kwa hiyo hasira ya Bwana inawaka dhidi ya watu wake,
mkono wake umeinuliwa na anawapiga.
Milima inatetemeka,
maiti ni kama takataka kwenye barabara.
Hata kwa haya yote, hasira yake haijageukia mbali,
mkono wake bado umeinuliwa juu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.