Isaya 5:1
Isaiah 5:1 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Nitaimba wimbo kwa ajili ya mmoja nimpendaye, kuhusu shamba lake la mizabibu: Mpendwa wangu alikuwa na shamba la mizabibu kwenye kilima chenye rutuba.
Isaiah 5:1 in English
Isaiah 5:1 · Berean Standard Bible
I will sing for my beloved a song of his vineyard: My beloved had a vineyard on a very fertile hill.
Context
1Nitaimba wimbo kwa ajili ya mmoja nimpendaye,
kuhusu shamba lake la mizabibu:
Mpendwa wangu alikuwa na shamba la mizabibu
kwenye kilima chenye rutuba. 2Alililima na kuondoa mawe
na akaliotesha mizabibu bora sana.
Akajenga mnara wa ulinzi ndani yake,
na kutengeneza shinikizo la kukamulia divai pia.
Kisha akatazamia kupata mazao ya zabibu nzuri,
lakini lilizaa matunda mabaya tu. 3“Basi enyi wakazi wa Yerusalemu na watu wa Yuda,
hukumuni kati yangu na shamba langu la mizabibu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.