Isaya 49:16
Isaiah 49:16 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Tazama, nimekuchora kama muhuri katika vitanga vya mikono yangu, kuta zako zi mbele yangu daima.
Isaiah 49:16 in English
Isaiah 49:16 · Berean Standard Bible
Behold, I have inscribed you on the palms of My hands; your walls are ever before Me.
Context
14Lakini Sayuni alisema, “Bwana ameniacha,
Bwana amenisahau.” 15“Je, mama aweza kumsahau mtoto
aliyeko matitini mwake akinyonya,
wala asiwe na huruma
juu ya mtoto aliyemzaa?
Ingawa anaweza kusahau,
mimi sitakusahau wewe! 16Tazama, nimekuchora kama muhuri
katika vitanga vya mikono yangu,
kuta zako zi mbele yangu daima. 17Wana wako wanaharakisha kurudi,
nao wale waliokuteka wanaondoka kwako. 18Inua macho yako ukatazame pande zote:
wana wako wote wanakusanyika na kukujia.
Kwa hakika kama vile niishivyo,
utawavaa wote kama mapambo,
na kujifunga nao kama bibi arusi,”
asema Bwana.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.