Isaya 48:12
Isaiah 48:12 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Ee Yakobo, nisikilize mimi, Israeli, ambaye nimekuita: Mimi ndiye; mimi ndimi mwanzo na mwisho.
Isaiah 48:12 in English
Isaiah 48:12 · Berean Standard Bible
Listen to Me, O Jacob, and Israel, whom I have called: I am He; I am the first, and I am the last.
Context
10Tazama, nimekusafisha, ingawa si kama fedha,
nimekujaribu katika tanuru ya mateso. 11Kwa ajili yangu mwenyewe,
kwa ajili yangu mwenyewe, nafanya hili.
Jinsi gani niliache Jina langu lichafuliwe?
Sitautoa utukufu wangu kwa mwingine. 12“Ee Yakobo, nisikilize mimi,
Israeli, ambaye nimekuita:
Mimi ndiye;
mimi ndimi mwanzo na mwisho. 13Mkono wangu mwenyewe uliweka misingi ya dunia,
nao mkono wangu wa kuume umezitanda mbingu;
niziitapo, zote husimama pamoja. 14“Kusanyikeni, ninyi nyote, msikilize:
Ni ipi miongoni mwa hizo sanamu
ambayo imetabiri vitu hivi?
Watu wa Bwana waliochaguliwa na kuungana
watatimiza kusudi lake dhidi ya Babeli;
mkono wa Mungu utakuwa dhidi ya Wakaldayo.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.