Isaya 48:10
Isaiah 48:10 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Tazama, nimekusafisha, ingawa si kama fedha, nimekujaribu katika tanuru ya mateso.
Isaiah 48:10 in English
Isaiah 48:10 · Berean Standard Bible
See, I have refined you, but not as silver; I have tested you in the furnace of affliction.
Context
8Hujayasikia wala kuyaelewa,
tangu zamani sikio lako halikufunguka.
Ninafahamu vyema jinsi ulivyo mdanganyifu,
uliitwa mwasi tangu kuzaliwa kwako. 9Kwa ajili ya Jina langu mwenyewe
ninaichelewesha ghadhabu yangu,
kwa ajili ya sifa zangu nimeizuia isikupate,
ili nisije nikakukatilia mbali. 10Tazama, nimekusafisha, ingawa si kama fedha,
nimekujaribu katika tanuru ya mateso. 11Kwa ajili yangu mwenyewe,
kwa ajili yangu mwenyewe, nafanya hili.
Jinsi gani niliache Jina langu lichafuliwe?
Sitautoa utukufu wangu kwa mwingine. 12“Ee Yakobo, nisikilize mimi,
Israeli, ambaye nimekuita:
Mimi ndiye;
mimi ndimi mwanzo na mwisho.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.