Isaya 46:8
Isaiah 46:8 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Kumbukeni hili, litieni akilini, liwekeni moyoni, enyi waasi.
Isaiah 46:8 in English
Isaiah 46:8 · Berean Standard Bible
Remember this and be brave; take it to heart, you transgressors!
Context
6Wengine humwaga dhahabu kutoka kwenye mifuko yao,
na kupima fedha kwenye mizani;
huajiri mfua dhahabu kutengeneza mungu,
kisha huisujudia na kuiabudu. 7Huiinua mabegani na kuichukua;
huiweka mahali pake, papo hapo ndipo isimamapo.
Wala haiwezi kusogea kutoka mahali pale.
Ingawa mtu huililia, haimjibu;
haiwezi kumwokoa kwenye taabu zake. 8“Kumbukeni hili, litieni akilini,
liwekeni moyoni, enyi waasi. 9Kumbukeni mambo yaliyopita, yale ya zamani za kale;
mimi ndimi Mungu, wala hakuna mwingine;
mimi ndimi Mungu,
wala hakuna mwingine aliye kama mimi. 10Ni mimi nitangazaye mwisho tangu mwanzo,
naam, tangu zamani za kale,
mambo ambayo hayajatendeka.
Ninasema: Kusudi langu ndilo litakalosimama,
nami nitatenda mapenzi yangu yote.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.