Isaya 46:6
Isaiah 46:6 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Wengine humwaga dhahabu kutoka kwenye mifuko yao, na kupima fedha kwenye mizani; huajiri mfua dhahabu kutengeneza mungu, kisha huisujudia na kuiabudu.
Isaiah 46:6 in English
Isaiah 46:6 · Berean Standard Bible
They pour out their bags of gold and weigh out silver on scales; they hire a goldsmith to fashion it into a god, so they can bow down and worship.
Context
4Hata mpaka wakati wa uzee wenu na mvi, Mimi ndiye,
Mimi ndiye nitakayewasaidia ninyi.
Nimewahuluku, nami nitawabeba,
nitawasaidia ninyi na kuwaokoa. 5“Mtanilinganisha na nani, au mtanihesabu kuwa sawa na nani?
Ni nani mtakayenifananisha naye ili tuweze kulinganishwa? 6Wengine humwaga dhahabu kutoka kwenye mifuko yao,
na kupima fedha kwenye mizani;
huajiri mfua dhahabu kutengeneza mungu,
kisha huisujudia na kuiabudu. 7Huiinua mabegani na kuichukua;
huiweka mahali pake, papo hapo ndipo isimamapo.
Wala haiwezi kusogea kutoka mahali pale.
Ingawa mtu huililia, haimjibu;
haiwezi kumwokoa kwenye taabu zake. 8“Kumbukeni hili, litieni akilini,
liwekeni moyoni, enyi waasi.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.