Isaya 45:22
Isaiah 45:22 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Nigeukieni mimi, nanyi mkaokolewe, enyi miisho yote ya dunia; kwa maana mimi ndimi Mungu, wala hapana mwingine.
Isaiah 45:22 in English
Isaiah 45:22 · Berean Standard Bible
Turn to Me and be saved, all the ends of the earth; for I am God, and there is no other.
Context
20“Kusanyikeni pamoja mje,
enyi wakimbizi kutoka mataifa.
Wale wabebao sanamu za mti ni watu wasio na akili,
wale waombao miungu isiyoweza kuokoa. 21Tangazeni litakalokuwepo, lisemeni hilo,
wao na wafanye shauri pamoja.
Ni nani aliyetangulia kusema hili tangu zamani,
aliyetangaza tangu zamani za kale?
Je, haikuwa Mimi, Bwana?
Wala hapana Mungu mwingine
zaidi yangu mimi,
Mungu mwenye haki na Mwokozi;
hapana mwingine ila mimi. 22“Nigeukieni mimi, nanyi mkaokolewe,
enyi miisho yote ya dunia;
kwa maana mimi ndimi Mungu,
wala hapana mwingine. 23Nimeapa kwa nafsi yangu,
kinywa changu kimenena katika uadilifu wote
neno ambalo halitatanguka:
Kila goti litapigwa mbele zangu,
kwangu mimi kila ulimi utaapa. 24Watasema kuhusu mimi,
‘Katika Bwana peke yake
ndiko kuna haki na nguvu.’ ”
Wote ambao wamemkasirikia Mungu
watamjia yeye, nao watatahayarika.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.