Isaya 42:17
Isaiah 42:17 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Lakini wale wanaotumaini sanamu, wanaoviambia vinyago, ‘Ninyi ndio miungu yetu,’ watarudishwa nyuma kwa aibu kubwa.
Isaiah 42:17 in English
Isaiah 42:17 · Berean Standard Bible
But those who trust in idols and say to molten images, ‘You are our gods!’ will be turned back in utter shame.
Context
15Nitaharibu milima na vilima
na kukausha mimea yako yote;
nitafanya mito kuwa visiwa
na kukausha mabwawa. 16Nitawaongoza vipofu kwenye njia ambayo hawajaijua,
kwenye mapito wasiyoyazoea nitawaongoza;
nitafanya giza kuwa nuru mbele yao,
na kufanya mahali palipoparuza kuwa laini.
Haya ndiyo mambo nitakayofanya;
mimi sitawaacha. 17Lakini wale wanaotumaini sanamu,
wanaoviambia vinyago, ‘Ninyi ndio miungu yetu,’
watarudishwa nyuma kwa aibu kubwa. 18“Sikieni, enyi viziwi;
tazameni, enyi vipofu, mpate kuona! 19Ni nani aliye kipofu isipokuwa mtumishi wangu,
na kiziwi kama mjumbe ninayemtuma?
Ni nani aliye kipofu kama yeye aliyejitoa kwangu,
aliye kipofu kama mtumishi wa Bwana?
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.