Native Bible

Isaiah 35:5 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Ndipo macho ya vipofu yatafumbuliwa na masikio ya viziwi yatazibuliwa.

Isaiah 35:5 in English

Isaiah 35:5 · Berean Standard Bible

Then the eyes of the blind will be opened and the ears of the deaf unstopped.

Context

3Itieni nguvu mikono iliyo dhaifu, yafanyeni imara magoti yaliyolegea, 4waambieni wale wenye mioyo ya hofu, “Kuweni hodari, msiogope; tazama, Mungu wenu atakuja, pamoja na malipo ya Mungu, atakuja na kuwaokoa ninyi.” 5Ndipo macho ya vipofu yatafumbuliwa na masikio ya viziwi yatazibuliwa. 6Ndipo kilema atarukaruka kama kulungu, nao ulimi wa aliye bubu utapaza sauti kwa shangwe. Maji yatatiririka kwa kasi katika nyika, na vijito katika jangwa. 7Mchanga wa moto utakuwa bwawa la maji, ardhi yenye kiu itabubujika chemchemi. Maskani ya mbweha walikolala hapo awali patamea majani, matete na mafunjo.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.