Isaya 32:12
Isaiah 32:12 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Pigeni matiti yenu kwa ajili ya mashamba mazuri, kwa ajili ya mizabibu iliyozaa vizuri
Isaiah 32:12 in English
Isaiah 32:12 · Berean Standard Bible
Beat your breasts for the pleasant fields, for the fruitful vines,
Context
10Muda zaidi kidogo ya mwaka mmoja,
ninyi mnaojisikia salama mtatetemeka,
mavuno ya zabibu yatakoma
na mavuno ya matunda hayatakuwepo. 11Tetemekeni, enyi wanawake wenye kuridhika,
tetemekeni kwa hofu, enyi binti mnaojisikia salama!
Vueni nguo zenu,
vaeni nguo ya gunia viunoni mwenu. 12Pigeni matiti yenu kwa ajili ya mashamba mazuri,
kwa ajili ya mizabibu iliyozaa vizuri 13na kwa ajili ya nchi ya watu wangu,
nchi ambayo miiba na michongoma imemea:
naam, ombolezeni kwa ajili ya nyumba zote za furaha
na kwa ajili ya mji huu wenye kufanya sherehe. 14Ngome itaachwa,
mji wenye kelele nyingi utahamwa,
ngome ndani ya mji na mnara wa ulinzi vitakuwa ukiwa milele,
mahali pazuri pa punda na malisho ya makundi ya kondoo,
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.