Native Bible

Isaiah 30:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Lakini ulinzi wa Farao utakuwa kwa aibu yenu, kivuli cha Misri kitawaletea fedheha.

Isaiah 30:3 in English

Isaiah 30:3 · Berean Standard Bible

But Pharaoh’s protection will become your shame, and the refuge of Egypt’s shade your disgrace.

Context

1Bwana asema, “Ole kwa watoto wakaidi, kwa wale wanaotimiza mipango ambayo si yangu, wakifanya makubaliano, lakini si kwa Roho wangu, wakilundika dhambi juu ya dhambi, 2wale washukao kwenda Misri bila kutaka shauri langu, wanaotafuta msaada wa ulinzi wa Farao, watafutao kivuli cha Misri kwa ajili ya kimbilio. 3Lakini ulinzi wa Farao utakuwa kwa aibu yenu, kivuli cha Misri kitawaletea fedheha. 4Ingawa wana maafisa katika Soani na wajumbe wamewasili katika Hanesi, 5kila mmoja ataaibishwa kwa sababu ya taifa lisilowafaa kitu, ambalo haliwaletei msaada wala faida, bali aibu tu na fedheha.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.