Isaya 29:17
Isaiah 29:17 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kwa muda mfupi sana, je, Lebanoni haitageuzwa kuwa shamba lenye rutuba, na shamba lenye rutuba liwe kama msitu?
Isaiah 29:17 in English
Isaiah 29:17 · Berean Standard Bible
In a very short time, will not Lebanon become an orchard, and the orchard seem like a forest?
Context
15Ole kwa wale wanaokwenda kwenye vilindi virefu
kumficha Bwana mipango yao,
wafanyao kazi zao gizani na kufikiri,
“Ni nani anayetuona? Ni nani atakayejua?” 16Mnapindua mambo juu chini,
kana kwamba mfinyanzi aweza kufikiriwa kuwa kama udongo wa mfinyanzi!
Je, kile kilichofinyangwa chaweza kumwambia yule aliyekifinyanga,
“Wewe hukunifinyanga mimi?”
Je, chungu kinaweza kumwambia mfinyanzi,
“Wewe hujui chochote?” 17Kwa muda mfupi sana, je, Lebanoni haitageuzwa kuwa shamba lenye rutuba,
na shamba lenye rutuba liwe kama msitu? 18Katika siku ile viziwi watasikia maneno ya kitabu,
na katika utusitusi na giza
macho ya kipofu yataona. 19Mara nyingine tena wanyenyekevu watafurahi katika Bwana,
wahitaji watafurahi katika yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.