Isaya 29:15
Isaiah 29:15 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ole kwa wale wanaokwenda kwenye vilindi virefu kumficha Bwana mipango yao, wafanyao kazi zao gizani na kufikiri, “Ni nani anayetuona? Ni nani atakayejua?”
Isaiah 29:15 in English
Isaiah 29:15 · Berean Standard Bible
Woe to those who dig deep to hide their plans from the LORD. In darkness they do their works and say, “Who sees us, and who will know?”
Context
13Bwana anasema:
“Watu hawa hunikaribia kwa vinywa vyao
na kuniheshimu kwa midomo yao,
lakini mioyo yao iko mbali nami.
Ibada yao kwangu inatokana na maagizo
waliyofundishwa na wanadamu. 14Kwa hiyo mara nyingine tena nitawashangaza watu hawa,
kwa ajabu juu ya ajabu.
Hekima ya wenye hekima itapotea,
nayo akili ya wenye akili itatoweka.” 15Ole kwa wale wanaokwenda kwenye vilindi virefu
kumficha Bwana mipango yao,
wafanyao kazi zao gizani na kufikiri,
“Ni nani anayetuona? Ni nani atakayejua?” 16Mnapindua mambo juu chini,
kana kwamba mfinyanzi aweza kufikiriwa kuwa kama udongo wa mfinyanzi!
Je, kile kilichofinyangwa chaweza kumwambia yule aliyekifinyanga,
“Wewe hukunifinyanga mimi?”
Je, chungu kinaweza kumwambia mfinyanzi,
“Wewe hujui chochote?” 17Kwa muda mfupi sana, je, Lebanoni haitageuzwa kuwa shamba lenye rutuba,
na shamba lenye rutuba liwe kama msitu?
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.