Isaya 28:8
Isaiah 28:8 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Meza zote zimejawa na matapishi wala hakuna sehemu hata ndogo isiyokuwa na uchafu.
Isaiah 28:8 in English
Isaiah 28:8 · Berean Standard Bible
For all their tables are covered with vomit; there is not a place without filth.
Context
6Atakuwa roho ya haki
kwa yeye aketiye katika kiti cha hukumu,
chanzo cha nguvu
kwa wale wazuiao vita langoni. 7Hawa pia wanapepesuka kwa sababu ya mvinyo,
wanayumbayumba kwa sababu ya kileo:
Makuhani na manabii wanapepesuka kwa sababu ya kileo,
wanachanganyikiwa kwa sababu ya mvinyo;
wanapepesuka wanapoona maono,
wanajikwaa wanapotoa maamuzi. 8Meza zote zimejawa na matapishi
wala hakuna sehemu hata ndogo
isiyokuwa na uchafu. 9“Yeye anajaribu kumfundisha nani?
Yeye anamwelezea nani ujumbe wake?
Je, ni kwa watoto walioachishwa kunyonya?
Je, ni wale ambao ndipo tu wametolewa matitini? 10Kwa maana ni:
Amri juu ya amri, amri juu ya amri,
kanuni juu ya kanuni, kanuni juu ya kanuni;
hapa kidogo, kule kidogo.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.