Isaya 28:20
Isaiah 28:20 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kitanda ni kifupi mno kujinyoosha juu yake, nguo ya kujifunikia ni nyembamba mno mtu hawezi kujifunikia.
Isaiah 28:20 in English
Isaiah 28:20 · Berean Standard Bible
Indeed, the bed is too short to stretch out on, and the blanket too small to wrap around you.
Context
18Agano lenu na kifo litabatilishwa,
patano lenu na kuzimu halitasimama.
Wakati pigo lifurikalo litakapowakumba,
litawaangusha chini. 19Kila mara lijapo litawachukua,
asubuhi baada ya asubuhi,
wakati wa mchana na wakati wa usiku,
litawakumba tangu mwanzo hadi mwisho.”
Kuuelewa ujumbe huu
utaleta hofu tupu. 20Kitanda ni kifupi mno kujinyoosha juu yake,
nguo ya kujifunikia ni nyembamba mno
mtu hawezi kujifunikia. 21Bwana atainuka kama alivyofanya kwenye Mlima Perasimu,
ataghadhibika kama alivyofanya katika Bonde la Gibeoni:
ili kufanya kazi yake, kazi yake ya ajabu,
ili kutimiza kazi yake, kazi yake ngeni. 22Sasa acheni dharau zenu,
la sivyo minyororo yenu itakuwa mizito zaidi.
Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote, ameniambia
habari za maangamizi yaliyoamriwa dhidi ya nchi yote.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.