Isaya 28:18
Isaiah 28:18 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Agano lenu na kifo litabatilishwa, patano lenu na kuzimu halitasimama. Wakati pigo lifurikalo litakapowakumba, litawaangusha chini.
Isaiah 28:18 in English
Isaiah 28:18 · Berean Standard Bible
Your covenant with death will be dissolved, and your agreement with Sheol will not stand. When the overwhelming scourge passes through, you will be trampled by it.
Context
16Kwa hiyo hivi ndivyo Bwana Mwenyezi asemavyo:
“Tazama, ninaweka jiwe katika Sayuni,
jiwe lililojaribiwa,
jiwe la pembeni la thamani kwa ajili ya msingi thabiti.
Yeye atumainiye kamwe hatatiwa hofu. 17Nitaifanya haki kuwa kamba ya kupimia
na uadilifu kuwa timazi;
mvua ya mawe itafagia kimbilio lenu, huo uongo,
nayo maji yatafurikia mahali penu pa kujificha. 18Agano lenu na kifo litabatilishwa,
patano lenu na kuzimu halitasimama.
Wakati pigo lifurikalo litakapowakumba,
litawaangusha chini. 19Kila mara lijapo litawachukua,
asubuhi baada ya asubuhi,
wakati wa mchana na wakati wa usiku,
litawakumba tangu mwanzo hadi mwisho.”
Kuuelewa ujumbe huu
utaleta hofu tupu. 20Kitanda ni kifupi mno kujinyoosha juu yake,
nguo ya kujifunikia ni nyembamba mno
mtu hawezi kujifunikia.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.