Isaya 27:12
Isaiah 27:12 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Katika siku ile Bwana atapura kutoka matiririko ya Mto Frati hadi Kijito cha Misri, nanyi ee Waisraeli, mtakusanywa mmoja mmoja.
Isaiah 27:12 in English
Isaiah 27:12 · Berean Standard Bible
In that day the LORD will thresh from the flowing Euphrates * to the Wadi of Egypt, and you, O Israelites, will be gathered one by one.
Context
10Mji ulio na boma umebaki ukiwa,
makao yaliyotelekezwa, yaliyoachwa kama jangwa.
Huko ndama hulisha,
huko hujilaza,
wanakwanyua matawi yake. 11Wakati vijiti vyake vimekauka, huvunjwa
nao wanawake huja na kuwasha navyo moto.
Kwa kuwa hili ni taifa lisilo na ufahamu,
kwa hiyo yeye aliyewafanya hana huruma juu yao,
Muumba wao hawaonyeshi fadhili. 12Katika siku ile Bwana atapura kutoka matiririko ya Mto Frati hadi Kijito cha Misri, nanyi ee Waisraeli, mtakusanywa mmoja mmoja. 13Katika siku ile tarumbeta kubwa italia. Wale waliokuwa wakiangamia katika nchi ya Ashuru, nao wale waliokuwa uhamishoni katika nchi ya Misri watakuja na kumwabudu Bwana katika mlima mtakatifu huko Yerusalemu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.