Isaya 27:10
Isaiah 27:10 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Mji ulio na boma umebaki ukiwa, makao yaliyotelekezwa, yaliyoachwa kama jangwa. Huko ndama hulisha, huko hujilaza, wanakwanyua matawi yake.
Isaiah 27:10 in English
Isaiah 27:10 · Berean Standard Bible
For the fortified city lies deserted— a homestead abandoned, a wilderness forsaken. There the calves graze, and there they lie down; they strip its branches bare.
Context
8Kwa vita na kwa kumfukuza unapingana naye:
kwa mshindo wake mkali anamfukuza,
kama siku ile uvumapo upepo wa mashariki. 9Kwa hili, basi, hatia ya Yakobo itafanyiwa upatanisho,
nalo hili litakuwa matunda ya utimilizo wa kuondolewa kwa dhambi yake:
Wakati atakapoyafanya mawe yote ya madhabahu
kuwa kama mawe ya chokaa yaliyopondwa vipande vipande,
hakuna nguzo za Ashera au madhabahu za kufukizia uvumba
zitakazobaki zimesimama. 10Mji ulio na boma umebaki ukiwa,
makao yaliyotelekezwa, yaliyoachwa kama jangwa.
Huko ndama hulisha,
huko hujilaza,
wanakwanyua matawi yake. 11Wakati vijiti vyake vimekauka, huvunjwa
nao wanawake huja na kuwasha navyo moto.
Kwa kuwa hili ni taifa lisilo na ufahamu,
kwa hiyo yeye aliyewafanya hana huruma juu yao,
Muumba wao hawaonyeshi fadhili. 12Katika siku ile Bwana atapura kutoka matiririko ya Mto Frati hadi Kijito cha Misri, nanyi ee Waisraeli, mtakusanywa mmoja mmoja.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.