Isaya 26:8
Isaiah 26:8 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Naam, Bwana, tukienenda katika sheria zako, twakungojea wewe, jina lako na sifa zako ndizo shauku za mioyo yetu.
Isaiah 26:8 in English
Isaiah 26:8 · Berean Standard Bible
Yes, we wait for You, O LORD; we walk in the path of Your judgments. Your name and renown are the desire of our souls.
Context
6Miguu huukanyaga chini,
miguu ya hao walioonewa,
hatua za hao maskini. 7Mapito ya wenye haki yamenyooka.
Ewe uliye Mwenye Haki,
waisawazisha njia ya mtu mnyofu. 8Naam, Bwana, tukienenda katika sheria zako,
twakungojea wewe,
jina lako na sifa zako
ndizo shauku za mioyo yetu. 9Nafsi yangu yakutamani wakati wa usiku,
wakati wa asubuhi roho yangu yakuonea shauku.
Wakati hukumu zako zinapokuja juu ya dunia,
watu wa ulimwengu hujifunza haki. 10Ingawa neema yaonyeshwa kwa waovu,
hawajifunzi haki,
hata katika nchi ya unyofu huendelea kutenda mabaya
wala hawazingatii utukufu wa Bwana.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.