Native Bible

Isaiah 26:6 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Miguu huukanyaga chini, miguu ya hao walioonewa, hatua za hao maskini.

Isaiah 26:6 in English

Isaiah 26:6 · Berean Standard Bible

Feet trample it down— the feet of the oppressed, the steps of the poor.

Context

4Mtumaini Bwana milele, kwa kuwa Bwana, Bwana, ni Mwamba wa milele. 5Huwashusha wale wajikwezao, huushusha chini mji wenye kiburi, huushusha hadi ardhini na kuutupa chini mavumbini. 6Miguu huukanyaga chini, miguu ya hao walioonewa, hatua za hao maskini. 7Mapito ya wenye haki yamenyooka. Ewe uliye Mwenye Haki, waisawazisha njia ya mtu mnyofu. 8Naam, Bwana, tukienenda katika sheria zako, twakungojea wewe, jina lako na sifa zako ndizo shauku za mioyo yetu.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.