Native Bible

Isaiah 24:17 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Hofu, shimo na mtego vinakungojea, ewe mtu ukaaye duniani.

Isaiah 24:17 in English

Isaiah 24:17 · Berean Standard Bible

Terror and pit and snare await you, O dweller of the earth.

Context

15Kwa hiyo upande wa mashariki mpeni Bwana utukufu, liadhimisheni jina la Bwana, Mungu wa Israeli, katika visiwa vya bahari. 16Kutoka miisho ya dunia tunasikia uimbaji: “Utukufu kwa Yule Mwenye Haki.” Lakini nilisema, “Ninadhoofika, ninadhoofika! Ole wangu! Watenda hila wanasaliti! Kwa hila watenda hila wanasaliti!” 17Hofu, shimo na mtego vinakungojea, ewe mtu ukaaye duniani. 18Kila akimbiaye asikiapo sauti ya hofu atatumbukia shimoni, naye yeyote apandaye kutoka shimoni, atanaswa kwenye mtego. Malango ya gharika ya mbinguni yamefunguliwa, misingi ya dunia inatikisika. 19Dunia imepasuka, dunia imechanika, dunia imetikiswa kabisa.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.