Isaya 24:15
Isaiah 24:15 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kwa hiyo upande wa mashariki mpeni Bwana utukufu, liadhimisheni jina la Bwana, Mungu wa Israeli, katika visiwa vya bahari.
Isaiah 24:15 in English
Isaiah 24:15 · Berean Standard Bible
Therefore glorify the LORD in the east. Extol the name of the LORD, the God of Israel in the islands * of the sea.
Context
13Ndivyo itakavyokuwa duniani
na miongoni mwa mataifa,
kama vile wakati mzeituni upigwavyo,
au kama vile wakati masazo yabakiavyo baada ya zabibu kuvunwa. 14Wanainua sauti zao, wanapiga kelele kwa furaha,
kutoka magharibi wanasifu kwa ukelele utukufu wa Bwana. 15Kwa hiyo upande wa mashariki mpeni Bwana utukufu,
liadhimisheni jina la Bwana, Mungu wa Israeli,
katika visiwa vya bahari. 16Kutoka miisho ya dunia tunasikia uimbaji:
“Utukufu kwa Yule Mwenye Haki.”
Lakini nilisema, “Ninadhoofika, ninadhoofika!
Ole wangu!
Watenda hila wanasaliti!
Kwa hila watenda hila wanasaliti!” 17Hofu, shimo na mtego vinakungojea,
ewe mtu ukaaye duniani.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.