Isaya 24:19
Isaiah 24:19 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Dunia imepasuka, dunia imechanika, dunia imetikiswa kabisa.
Isaiah 24:19 in English
Isaiah 24:19 · Berean Standard Bible
The earth is utterly broken apart, the earth is split open, the earth is shaken violently.
Context
17Hofu, shimo na mtego vinakungojea,
ewe mtu ukaaye duniani. 18Kila akimbiaye asikiapo sauti ya hofu
atatumbukia shimoni,
naye yeyote apandaye kutoka shimoni,
atanaswa kwenye mtego.
Malango ya gharika ya mbinguni yamefunguliwa,
misingi ya dunia inatikisika. 19Dunia imepasuka,
dunia imechanika,
dunia imetikiswa kabisa. 20Dunia inapepesuka kama mlevi,
inayumbayumba kama kibanda kwenye upepo;
imelemewa sana na mzigo wa hatia ya uasi wake
na ikianguka kamwe haitainuka tena. 21Katika siku ile Bwana ataadhibu
nguvu zilizoko mbinguni juu,
na wafalme walioko duniani chini.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.