Isaya 23:11
Isaiah 23:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Bwana amenyoosha mkono wake juu ya bahari na kuzifanya falme zake zitetemeke. Ametoa amri kuhusu Kanaani kwamba ngome zake ziangamizwe.
Isaiah 23:11 in English
Isaiah 23:11 · Berean Standard Bible
The LORD has stretched out His hand over the sea; He has made kingdoms tremble. He has given a command that the strongholds of Canaan be destroyed.
Context
9Bwana Mwenye Nguvu Zote ndiye alipanga jambo hili,
ili kukishusha kiburi cha utukufu wote
na kuwanyenyekesha wale wote
ambao ni mashuhuri duniani. 10Ee Binti Tarshishi,
pita katika nchi yako kama vile Mto Naili
kwa kuwa huna tena bandari. 11Bwana amenyoosha mkono wake juu ya bahari
na kuzifanya falme zake zitetemeke.
Ametoa amri kuhusu Kanaani
kwamba ngome zake ziangamizwe. 12Alisema, “Usizidi kufurahi,
ee Bikira Binti Sidoni, sasa umepondwa!
“Simama, vuka uende Kitimu;
hata huko hutapata pumziko.” 13Tazama katika nchi ya Wakaldayo,
watu hawa ambao sasa hawaonekani kama wapo!
Waashuru wameifanya nchi hiyo
kuwa mahali pa viumbe wa jangwani.
Wamesimamisha minara yao ya vita kuuzunguka,
wameziteka ngome zake na kuziacha tupu
na kuufanya kuwa magofu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.