Isaya 22:20
Isaiah 22:20 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Katika siku ile, nitamwita mtumishi wangu, Eliakimu mwana wa Hilkia.
Isaiah 22:20 in English
Isaiah 22:20 · Berean Standard Bible
On that day I will summon My servant, Eliakim son of Hilkiah.
Context
18Atakuvingirisha uwe kama mpira
na kukutupa katika nchi kubwa.
Huko ndiko utakakofia,
na huko ndiko magari yako ya vita ya fahari yatabakia,
wewe unayeifedhehesha nyumba ya bwana wako! 19Nitakuondoa kutoka kazi yako,
nawe utaondoshwa kutoka nafasi yako. 20“Katika siku ile, nitamwita mtumishi wangu, Eliakimu mwana wa Hilkia. 21Nitamvika joho lako, nami nitamfunga mshipi wako kiunoni mwake, na kumkabidhi mamlaka yako. Yeye atakuwa baba kwa wale wanaoishi Yerusalemu na kwa nyumba ya Yuda. 22Nitaweka mabegani mwake ufunguo wa nyumba ya Daudi. Kile afunguacho hakuna awezaye kufunga, na kile afungacho hakuna awezaye kufungua.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.