Isaya 2:9
Isaiah 2:9 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kwa hiyo mwanadamu atashushwa na binadamu atanyenyekezwa: usiwasamehe.
Isaiah 2:9 in English
Isaiah 2:9 · Berean Standard Bible
So mankind is brought low, and man is humbled— do not forgive them!
Context
7Nchi yao imejaa fedha na dhahabu,
hakuna mwisho wa hazina zao.
Nchi yao imejaa farasi,
hakuna mwisho wa magari yao. 8Nchi yao imejaa sanamu,
wanasujudia kazi za mikono yao,
vitu vile vidole vyao vimevitengeneza. 9Kwa hiyo mwanadamu atashushwa
na binadamu atanyenyekezwa:
usiwasamehe. 10Ingieni kwenye miamba,
jificheni ardhini
kutokana na utisho wa Bwana
na utukufu wa enzi yake! 11Macho ya mtu mwenye majivuno yatanyenyekezwa
na kiburi cha wanadamu kitashushwa,
Bwana peke yake ndiye atakayetukuzwa siku hiyo.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.