Isaya 2:5
Isaiah 2:5 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Njooni, enyi nyumba ya Yakobo, tutembeeni katika nuru ya Bwana.
Isaiah 2:5 in English
Isaiah 2:5 · Berean Standard Bible
Come, O house of Jacob, let us walk in the light of the LORD.
Context
3Mataifa mengi yatakuja na kusema,
“Njooni, twendeni mlimani mwa Bwana,
kwenye nyumba ya Mungu wa Yakobo.
Atatufundisha njia zake,
ili tuweze kuenenda katika mapito yake.”
Sheria itatoka Sayuni,
neno la Bwana litatoka Yerusalemu. 4Atahukumu kati ya mataifa
na ataamua migogoro ya mataifa mengi.
Watafua panga zao ziwe majembe,
na mikuki yao kuwa miundu ya kukata matawi.
Taifa halitainua upanga dhidi ya taifa jingine,
wala hawatajifunza vita tena. 5Njooni, enyi nyumba ya Yakobo,
tutembeeni katika nuru ya Bwana. 6Umewatelekeza watu wako,
nyumba ya Yakobo.
Wamejaa ushirikina utokao Mashariki,
wanapiga ramli kama Wafilisti
na wanashikana mikono na wapagani. 7Nchi yao imejaa fedha na dhahabu,
hakuna mwisho wa hazina zao.
Nchi yao imejaa farasi,
hakuna mwisho wa magari yao.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.