Native Bible

Isaiah 19:5 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Maji ya mito yatakauka, chini ya mto kutakauka kwa jua.

Isaiah 19:5 in English

Isaiah 19:5 · Berean Standard Bible

The waters of the Nile will dry up, and the riverbed will be parched and empty.

Context

3Wamisri watakufa moyo, na nitaibatilisha mipango yao. Watatafuta ushauri kwa sanamu na kwa roho za waliokufa, kwa waaguzi na kwa wale waongeao na mizimu. 4Nitawatia Wamisri mikononi mwa bwana mkatili na mfalme mkali atatawala juu yao,” asema Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote. 5Maji ya mito yatakauka, chini ya mto kutakauka kwa jua. 6Mifereji itanuka; vijito vya Misri vitapungua na kukauka. Mafunjo na nyasi vitanyauka, 7pia mimea iliyoko kando ya Mto Naili, pale mto unapomwaga maji baharini. Kila shamba lililopandwa kando ya Mto Naili litakauka, litapeperushwa na kutoweka kabisa.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.