Native Bible

Isaiah 19:6 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Mifereji itanuka; vijito vya Misri vitapungua na kukauka. Mafunjo na nyasi vitanyauka,

Isaiah 19:6 in English

Isaiah 19:6 · Berean Standard Bible

The canals will stink; the streams of Egypt will trickle and dry up; the reeds and rushes will wither.

Context

4Nitawatia Wamisri mikononi mwa bwana mkatili na mfalme mkali atatawala juu yao,” asema Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote. 5Maji ya mito yatakauka, chini ya mto kutakauka kwa jua. 6Mifereji itanuka; vijito vya Misri vitapungua na kukauka. Mafunjo na nyasi vitanyauka, 7pia mimea iliyoko kando ya Mto Naili, pale mto unapomwaga maji baharini. Kila shamba lililopandwa kando ya Mto Naili litakauka, litapeperushwa na kutoweka kabisa. 8Wavuvi watalia na kuomboleza, wale wote watupao ndoano katika Mto Naili, watadhoofika kwa majonzi.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.