Native Bible

Isaiah 17:6 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Hata hivyo baadhi ya masazo yatabaki, kama vile mti wa mzeituni unavyopigwa, kukiachwa zeituni mbili au tatu juu ya matawi kileleni, nne au tano katika matawi yazaayo sana,” asema Bwana, Mungu wa Israeli.

Isaiah 17:6 in English

Isaiah 17:6 · Berean Standard Bible

Yet gleanings will remain, like an olive tree that has been beaten— two or three berries atop the tree, four or five on its fruitful branches,” declares the LORD, the God of Israel.

Context

4“Katika siku ile utukufu wa Yakobo utafifia, unono wa mwili wake utadhoofika. 5Itakuwa kama mvunaji akusanyavyo nafaka na kuvuna nafaka kwa mikono yake, kama wakati mtu aokotapo masazo ya masuke katika Bonde la Warefai. 6Hata hivyo baadhi ya masazo yatabaki, kama vile mti wa mzeituni unavyopigwa, kukiachwa zeituni mbili au tatu juu ya matawi kileleni, nne au tano katika matawi yazaayo sana,” asema Bwana, Mungu wa Israeli. 7Katika siku ile watu watamwangalia Muumba wao, na kuelekeza macho yao kwa yule Aliye Mtakatifu wa Israeli. 8Hawataziangalia tena madhabahu, kazi za mikono yao, nao hawataheshimu nguzo za Ashera,* na madhabahu za kufukizia uvumba zilizofanywa kwa mikono yao.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.