Native Bible

Isaiah 17:7 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Katika siku ile watu watamwangalia Muumba wao, na kuelekeza macho yao kwa yule Aliye Mtakatifu wa Israeli.

Isaiah 17:7 in English

Isaiah 17:7 · Berean Standard Bible

In that day men will look to their Maker and turn their eyes to the Holy One of Israel.

Context

5Itakuwa kama mvunaji akusanyavyo nafaka na kuvuna nafaka kwa mikono yake, kama wakati mtu aokotapo masazo ya masuke katika Bonde la Warefai. 6Hata hivyo baadhi ya masazo yatabaki, kama vile mti wa mzeituni unavyopigwa, kukiachwa zeituni mbili au tatu juu ya matawi kileleni, nne au tano katika matawi yazaayo sana,” asema Bwana, Mungu wa Israeli. 7Katika siku ile watu watamwangalia Muumba wao, na kuelekeza macho yao kwa yule Aliye Mtakatifu wa Israeli. 8Hawataziangalia tena madhabahu, kazi za mikono yao, nao hawataheshimu nguzo za Ashera,* na madhabahu za kufukizia uvumba zilizofanywa kwa mikono yao. 9Katika siku ile miji yao iliyo imara, ambayo waliihama kwa sababu ya Waisraeli, itakuwa kama mahali palipoachwa pa vichaka na magugu. Nayo yote itakuwa ukiwa.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.