Isaya 16:11
Isaiah 16:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Moyo wangu unaomboleza kwa ajili ya Moabu kama kinubi, nafsi yangu yote kwa ajili ya Kir-Haresethi.
Isaiah 16:11 in English
Isaiah 16:11 · Berean Standard Bible
Therefore my heart laments for Moab like a harp, my inmost being for Kir-heres.*
Context
9Hivyo ninalia kama Yazeri aliavyo,
kwa ajili ya mizabibu ya Sibma.
Ee Heshboni, ee Eleale,
ninakulowesha kwa machozi!
Kelele za furaha kwa ajili ya tunda lako lililoiva
na kwa ajili ya mavuno zimekomeshwa. 10Furaha na shangwe zimeondolewa
kutoka mashamba ya matunda;
hakuna yeyote aimbaye wala apazaye sauti
katika mashamba ya mizabibu;
hakuna yeyote akanyagaye zabibu shinikizoni,
kwa kuwa nimekomesha makelele. 11Moyo wangu unaomboleza kwa ajili ya Moabu kama kinubi,
nafsi yangu yote kwa ajili ya Kir-Haresethi. 12Wakati Moabu anapojitokeza mahali pake pa juu,
anajichosha mwenyewe tu;
anapokwenda mahali pake pa kuabudia miungu ili kuomba,
haitamfaidi lolote. 13Hili ndilo neno ambalo Bwana ameshasema kuhusu Moabu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.