Isaya 14:7
Isaiah 14:7 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Nchi zote ziko kwenye mapumziko na kwenye amani, wanabubujika kwa kuimba.
Isaiah 14:7 in English
Isaiah 14:7 · Berean Standard Bible
All the earth is at peace and at rest; they break out in song.
Context
5Bwana amevunja fimbo ya mwovu,
fimbo ya utawala ya watawala, 6ambayo kwa hasira waliyapiga mataifa
kwa mapigo yasiyo na kikomo,
nao kwa ghadhabu kali waliwatiisha mataifa
kwa jeuri pasipo huruma. 7Nchi zote ziko kwenye mapumziko na kwenye amani,
wanabubujika kwa kuimba. 8Hata misunobari na mierezi ya Lebanoni
inashangilia mbele yako na kusema,
“Basi kwa sababu umeangushwa chini,
hakuna mkata miti atakayekuja kutukata.” 9Kuzimu kote kumetaharuki
kukulaki unapokuja,
kunaamsha roho za waliokufa ili kukupokea,
wote waliokuwa viongozi katika ulimwengu,
kunawafanya wainuke kwenye viti vyao vya kifalme:
wale wote waliokuwa wafalme juu ya mataifa.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.