Native Bible

Isaiah 13:2 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Twekeni bendera juu ya mlima usio na kitu, wapazieni sauti, wapungieni mkono waingie katika malango ya wenye heshima.

Isaiah 13:2 in English

Isaiah 13:2 · Berean Standard Bible

Raise a banner on a barren hilltop; call aloud to them. Wave your hand, that they may enter the gates of the nobles.

Context

1Neno kuhusu Babeli ambalo Isaya mwana wa Amozi aliliona: 2Twekeni bendera juu ya mlima usio na kitu, wapazieni sauti, wapungieni mkono waingie katika malango ya wenye heshima. 3Nimewaamuru watakatifu wangu; nimewaita mashujaa wangu waitimize hasira yangu: wale wanaoshangilia ushindi wangu. 4Sikilizeni kelele juu ya milima, kama ile ya umati mkubwa wa watu! Sikilizeni, makelele katikati ya falme, kama mataifa yanayokusanyika pamoja! Bwana Mwenye Nguvu Zote anakusanya jeshi kwa ajili ya vita.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.