Native Bible

Isaiah 10:8 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Maana asema, ‘Je, wafalme wote si majemadari wangu?

Isaiah 10:8 in English

Isaiah 10:8 · Berean Standard Bible

“Are not all my commanders kings?” he says.

Context

6Ninamtuma dhidi ya taifa lisilomjua Mungu, ninamtuma dhidi ya taifa linalonikasirisha, kukamata mateka na kunyakua nyara, pia kuwakanyaga chini kama matope ya barabarani. 7Lakini hili silo analokusudia, hili silo alilo nalo akilini; kusudi lake ni kuangamiza, kuyakomesha mataifa mengi. 8Maana asema, ‘Je, wafalme wote si majemadari wangu? 9Je, Kalno hakutendwa kama Karkemishi? Hamathi si kama Arpadi, nayo Samaria si kama Dameski? 10Kama vile mkono wangu ulivyotwaa falme za sanamu, falme ambazo vinyago vyao vilizidi vile vya Yerusalemu na Samaria:

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.