Isaya 10:24
Isaiah 10:24 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kwa hiyo, hili ndilo Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote asemalo: “Enyi watu wangu mkaao Sayuni, msiwaogope Waashuru, wanaowapiga ninyi kwa fimbo na kuinua rungu dhidi yenu, kama Misri ilivyofanya.
Isaiah 10:24 in English
Isaiah 10:24 · Berean Standard Bible
Therefore this is what the Lord GOD of Hosts says: “O My people who dwell in Zion, do not fear Assyria, who strikes you with a rod and lifts his staff against you as the Egyptians did.
Context
22Ingawa watu wako, ee Israeli, ni wengi kama mchanga wa pwani,
ni mabaki yao tu watakaorudi.
Maangamizi yamekwisha amriwa,
ni mengi tena ni haki. 23Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote, atatekeleza
maangamizi yaliyoamriwa juu ya nchi yote. 24Kwa hiyo, hili ndilo Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote asemalo:
“Enyi watu wangu mkaao Sayuni,
msiwaogope Waashuru,
wanaowapiga ninyi kwa fimbo
na kuinua rungu dhidi yenu, kama Misri ilivyofanya. 25Bado kitambo kidogo sana hasira yangu dhidi yenu itakoma,
na ghadhabu yangu itaelekezwa kwenye maangamizi yao.” 26Bwana Mwenye Nguvu Zote atawachapa kwa mjeledi,
kama alivyowapiga Wamidiani katika mwamba wa Orebu,
naye atainua fimbo yake juu ya maji,
kama alivyofanya huko Misri.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.