Isaya 10:26
Isaiah 10:26 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Bwana Mwenye Nguvu Zote atawachapa kwa mjeledi, kama alivyowapiga Wamidiani katika mwamba wa Orebu, naye atainua fimbo yake juu ya maji, kama alivyofanya huko Misri.
Isaiah 10:26 in English
Isaiah 10:26 · Berean Standard Bible
And the LORD of Hosts will brandish a whip against them, as when He struck Midian at the rock of Oreb. He will raise His staff over the sea, as He did in Egypt.
Context
24Kwa hiyo, hili ndilo Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote asemalo:
“Enyi watu wangu mkaao Sayuni,
msiwaogope Waashuru,
wanaowapiga ninyi kwa fimbo
na kuinua rungu dhidi yenu, kama Misri ilivyofanya. 25Bado kitambo kidogo sana hasira yangu dhidi yenu itakoma,
na ghadhabu yangu itaelekezwa kwenye maangamizi yao.” 26Bwana Mwenye Nguvu Zote atawachapa kwa mjeledi,
kama alivyowapiga Wamidiani katika mwamba wa Orebu,
naye atainua fimbo yake juu ya maji,
kama alivyofanya huko Misri. 27Katika siku hiyo mzigo wao utainuliwa kutoka mabegani mwenu,
na nira yao kutoka shingoni mwenu;
nira itavunjwa
kwa sababu ya kutiwa mafuta. 28Wanaingia Ayathi,
wanapita katikati ya Migroni,
wanahifadhi mahitaji huko Mikmashi.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.