Native Bible

Isaiah 1:7 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Nchi yenu imekuwa ukiwa, miji yenu imeteketezwa kwa moto; nchi yenu imeachwa tupu na wageni mbele ya macho yenu, imeharibiwa kama vile imepinduliwa na wageni.

Isaiah 1:7 in English

Isaiah 1:7 · Berean Standard Bible

Your land is desolate; your cities are burned with fire. Foreigners devour your fields before you— a desolation demolished by strangers.

Context

5Kwa nini mzidi kupigwa? Kwa nini kudumu katika uasi? Kichwa chako chote kimejeruhiwa, moyo wako wote ni mgonjwa. 6Kutoka wayo wako wa mguu hadi kwenye utosi wa kichwa chako hakuna uzima: ni majeraha matupu na makovu na vidonda vitokavyo damu, havikusafishwa au kufungwa wala kulainishwa kwa mafuta. 7Nchi yenu imekuwa ukiwa, miji yenu imeteketezwa kwa moto; nchi yenu imeachwa tupu na wageni mbele ya macho yenu, imeharibiwa kama vile imepinduliwa na wageni. 8Binti Sayuni ameachwa kama kipenu katika shamba la mizabibu, kama kibanda katika shamba la matikitimaji, kama mji uliohusuriwa. 9Kama Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote* asingelituachia walionusurika, tungelikuwa kama Sodoma, tungelifanana na Gomora.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.