Native Bible

Isaiah 1:9 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Kama Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote* asingelituachia walionusurika, tungelikuwa kama Sodoma, tungelifanana na Gomora.

Isaiah 1:9 in English

Isaiah 1:9 · Berean Standard Bible

Unless the LORD of Hosts had left us a few survivors,* we would have become like Sodom, we would have resembled Gomorrah.*

Context

7Nchi yenu imekuwa ukiwa, miji yenu imeteketezwa kwa moto; nchi yenu imeachwa tupu na wageni mbele ya macho yenu, imeharibiwa kama vile imepinduliwa na wageni. 8Binti Sayuni ameachwa kama kipenu katika shamba la mizabibu, kama kibanda katika shamba la matikitimaji, kama mji uliohusuriwa. 9Kama Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote* asingelituachia walionusurika, tungelikuwa kama Sodoma, tungelifanana na Gomora. 10Sikieni neno la Bwana, ninyi watawala wa Sodoma; sikilizeni sheria ya Mungu wetu, enyi watu wa Gomora! 11Bwana anasema, “Wingi wa sadaka zenu, ni kitu gani kwangu? Ninazo sadaka za kuteketezwa nyingi kupita kiasi, za kondoo dume na mafuta ya wanyama walionona. Sipendezwi na damu za mafahali wala za wana-kondoo na mbuzi.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.