Native Bible

Isaiah 1:10 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Sikieni neno la Bwana, ninyi watawala wa Sodoma; sikilizeni sheria ya Mungu wetu, enyi watu wa Gomora!

Isaiah 1:10 in English

Isaiah 1:10 · Berean Standard Bible

Hear the word of the LORD, you rulers of Sodom; listen to the instruction of our God, you people of Gomorrah!

Context

8Binti Sayuni ameachwa kama kipenu katika shamba la mizabibu, kama kibanda katika shamba la matikitimaji, kama mji uliohusuriwa. 9Kama Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote* asingelituachia walionusurika, tungelikuwa kama Sodoma, tungelifanana na Gomora. 10Sikieni neno la Bwana, ninyi watawala wa Sodoma; sikilizeni sheria ya Mungu wetu, enyi watu wa Gomora! 11Bwana anasema, “Wingi wa sadaka zenu, ni kitu gani kwangu? Ninazo sadaka za kuteketezwa nyingi kupita kiasi, za kondoo dume na mafuta ya wanyama walionona. Sipendezwi na damu za mafahali wala za wana-kondoo na mbuzi. 12Mnapokuja kujihudhurisha mbele zangu, ni nani aliyewataka ninyi mfanye hivyo, huku kuzikanyaga nyua zangu?

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.