Native Bible

Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Hata wakilea watoto, nitamuua kila mmoja. Ole wao nitakapowapiga kisogo!

Hosea 9:12 in English

Hosea 9:12 · Berean Standard Bible

Even if they raise their children, I will bereave them of each one. Yes, woe be to them when I turn away from them!

Context

10“Nilipompata Israeli, ilikuwa kama kupata zabibu jangwani; nilipowaona baba zenu, ilikuwa kama kuona matunda ya kwanza katika mtini. Lakini walipofika Baal-Peori, walijiweka wakfu kwa ile sanamu ya aibu, nao wakawa najisi kama kitu kile walichokipenda. 11Utukufu wa Efraimu utaruka kama ndege: hakuna kuzaa, hakuna kuchukua mimba, hakuna kutunga mimba. 12Hata wakilea watoto, nitamuua kila mmoja. Ole wao nitakapowapiga kisogo! 13Nimemwona Efraimu, kama Tiro, aliyeoteshwa mahali pazuri. Lakini Efraimu wataleta watoto wao kwa mchinjaji.” 14Wape, Ee Bwana, je, utawapa nini? Wape matumbo ya kuharibu mimba na matiti yaliyokauka.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.