Hosea 8:11
Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Ingawa Efraimu alijenga madhabahu nyingi kwa ajili ya sadaka za dhambi, hizi zimekuwa madhabahu za kufanyia dhambi.
Hosea 8:11 in English
Hosea 8:11 · Berean Standard Bible
Though Ephraim multiplied the altars for sin, they became his altars for sinning.
Context
9Kwa kuwa wamepanda kwenda Ashuru
kama punda-mwitu anayetangatanga peke yake.
Efraimu amejiuza mwenyewe
kwa wapenzi. 10Ingawa wamejiuza wenyewe miongoni mwa mataifa,
sasa nitawakusanya pamoja.
Wataanza kudhoofika chini ya uonevu
wa mfalme mwenye nguvu. 11“Ingawa Efraimu alijenga madhabahu nyingi
kwa ajili ya sadaka za dhambi,
hizi zimekuwa madhabahu
za kufanyia dhambi. 12Nimeandika kwa ajili yao mambo mengi
kuhusu sheria yangu,
lakini wameziangalia
kama kitu cha kigeni. 13Wanatoa dhabihu nilizopewa mimi
nao wanakula hiyo nyama,
lakini Bwana hapendezwi nao.
Sasa ataukumbuka uovu wao
na kuadhibu dhambi zao:
Watarudi Misri.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.