Hosea 7:5
Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Katika sikukuu ya mfalme wetu wakuu wanawaka kwa mvinyo, naye anawaunga mkono wenye mizaha.
Hosea 7:5 in English
Hosea 7:5 · Berean Standard Bible
The princes are inflamed with wine on the day of our king; so he joins hands with those who mock him.
Context
3“Wanamfurahisha sana mfalme kwa maovu yao,
wakuu wao kwa uongo wao. 4Wote ni wazinzi,
wanawaka kama tanuru
ambayo moto wake mwokaji hana haja ya kuuchochea
kuanzia kukanda unga
hadi umekwisha kuumuka. 5Katika sikukuu ya mfalme wetu
wakuu wanawaka kwa mvinyo,
naye anawaunga mkono wenye mizaha. 6Mioyo yao ni kama tanuru,
wanamwendea kwa hila.
Hasira yao inafoka moshi usiku kucha,
wakati wa asubuhi inalipuka
kama miali ya moto. 7Wote ni moto kama tanuru;
wanawaangamiza watawala wao.
Wafalme wake wote wanaanguka,
wala hakuna yeyote kati yao aniitaye mimi.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.