Hosea 7:10
Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kiburi cha Israeli kinashuhudia dhidi yake, lakini pamoja na haya yote harudi kwa Bwana Mungu wake wala kumtafuta.
Hosea 7:10 in English
Hosea 7:10 · Berean Standard Bible
Israel’s arrogance testifies against them, yet they do not return to the LORD their God; despite all this, they do not seek Him.
Context
8“Efraimu anajichanganya na mataifa;
Efraimu ni mkate ambao haukuiva. 9Wageni wananyonya nguvu zake,
lakini hafahamu hilo.
Nywele zake zina mvi hapa na pale,
lakini hana habari. 10Kiburi cha Israeli kinashuhudia dhidi yake,
lakini pamoja na haya yote
harudi kwa Bwana Mungu wake
wala kumtafuta. 11“Efraimu ni kama hua,
hudanganywa kwa urahisi na hana akili:
mara anaita Misri,
mara anageukia Ashuru. 12Wakati watakapokwenda,
nitatupa wavu wangu juu yao;
nitawavuta chini waanguke
kama ndege wa angani.
Nitakaposikia wakikusanyika pamoja,
nitawanasa.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.