Hosea 4:5
Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Unajikwaa usiku na mchana, nao manabii hujikwaa pamoja nawe. Kwa hiyo nitamwangamiza mama yako:
Hosea 4:5 in English
Hosea 4:5 · Berean Standard Bible
You will stumble by day, and the prophet will stumble with you by night; so I will destroy your mother—
Context
3Kwa sababu hii nchi huomboleza,
wote waishio ndani mwake wanadhoofika,
wanyama wa kondeni, ndege wa angani
na samaki wa baharini wanakufa. 4“Lakini mtu awaye yote na asilete shtaka,
mtu yeyote na asimlaumu mwenzake,
kwa maana watu wako ni kama wale
waletao mashtaka dhidi ya kuhani. 5Unajikwaa usiku na mchana,
nao manabii hujikwaa pamoja nawe.
Kwa hiyo nitamwangamiza mama yako: 6watu wangu wanaangamizwa
kwa kukosa maarifa,
“Kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa,
mimi nami nitakukataa wewe
usiwe kuhani kwangu mimi;
kwa kuwa umeacha kuijali sheria ya Mungu wako
mimi nami sitawajali watoto wako. 7Kadiri makuhani walivyoongezeka,
ndivyo walivyozidi kutenda dhambi dhidi yangu,
walibadilisha utukufu wao kwa kitu cha aibu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.